Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, January 30, 2022

Bodi Ya Utalii Tanzania –TTB Yapokea Maandamano Ya Vijana Wa Ccm Ya Kuhamasisha Utalii Wa Ndani.

 


Bodi ya utalii Tanzania (TTB)  imeapokea maandamano ya Wanachama wa Umoja wa Vijana –UVCCM Tanzania Kata ya Saranga iliyopo katika Jimbo la Kibamba, Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam ya kuhamasisha Utalii wa ndani hasa wa kupanda Mlima Kilimanjaro. Maandamano hayo yaliyoanzia katika kata ya Saranga na kupokelewa katika Export Processing Zones Authority (EPZA) na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa TTB Bw. Felix John.

Vijana hao ambao wamesema wanatekeleza ilani ya chama hicho ya kuvutia Watalii wa ndani na kuongeza pato la Taifa kupitia sekta hiyo, wameamua kuutangaza Mlima Kilimanjaro kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 45 tangu kuanzishwa kwa CCM.

Akizungumza mara baada ya kupokea maandamano hayo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTB Bw. Felix John amesema, mchango wa sekta ya utalii katika kukuza ajira kwa vijana ni mkubwa hivyo kufanyika kwa maandamano haya ya kuutangaza utalii ni sehemu mojawapo ya kuchochea uchumi wa Taifa , hivyo tunawapongeza vijana hawa kutuunga mkono katika kutangaza vivutio vyetu”.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Saranga Bw. Ally Adam Chinangu amesema “wameamua kuitangazia Dunia kuwa Mlima Kilimanjaro ni mali ya Tanzania, pamoja na kuwa unaweza kuuona ukiwa kwenye nchi jirani, Sisi vijana tunasema tuijulishe dunia kama Mlima  Kilimanjaro upo nchini Tanzania”.

Nao baadhi ya washiriki wanawake katika maandamano hayo kutoka Bodi ya Utalii Tanzania na UVCCM Kata ya Saranga, wametumia fursa ya maandamano hayo kuhamasisha Wanawake kutumia siku ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani inayoadhimishwa tarehe 8 mwezi wa tatu ya kila mwaka kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo nchini.

TTB inaendelea na juhudi za kuhamasisha utalii kwa makundi mbalimbali ya kijamii yakiwepo ya Vijana, Wawake, Wanafunzi na mengine mengi, katika kutembelea vivutio vya utalii na kuvitangaza ili kuvutia Watanzania kujenga utamaduni wa kuvitembelea vivutio hivyo.Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: