Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, January 4, 2022

CCM Pwani watoa tamko Spika Ndugai kuomba radhi


Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Chama Cha Mapinduzi (CCM ),Mkoani Pwani kimesema ,kitendo cha ujasiri alichokifanya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ,kukiri mapungufu baada ya taharuki ya kauli yake kuhusu mikopo wa Serikali si kujidharirisha bali ni kujiimaisha kisiasa kwa vitendo.


Akizungumza na waandishi wa habari , ofisini kwake,Mjini Kibaha Mwenyekiti wa CCM Mkoani Pwani , Ramadhani Maneno alieleza, kitendo cha Spika Ndugai kutoka hadharani kumuomba Radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Watanzania kijumla kutokana na kauli hiyo tata ni uungwana .


“Kutokana na taharuki hiyo aliyoitoa Ndugai ,takriban wiki moja kwa nchi na watanzania nachukua fursa hii kumpongeza kwa kuonyesha ujasiri kwa kumuomba Radhi Rais Samia Suluhu Hassan na Watanzania kijumla.”aliongeza Maneno.


Alimshukuru kwa kuwa jasiri kwani kukiri mapungufu si kujidharirisha ni kujiimaisha.
Maneno alisema kwamba,  ombi lake kwa WanaCCM waendelee kuamini kauli ya Spika na kuwa mstari wa mbele kumuunga mkono Rais na maendeleo ya nchi.


January 3 mwaka huu ,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai alimuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Watanzania wote baada ya kuhisiwa kuzungumza maneno ya kuvunja Moyo kuhusu Mikopo wa Serikali.


Spika Ndugai alieleza, hakukuwa na lolote la kurudisha nyuma juhudi za Serikali wala hakuwa na nia ya kukashifu, kudharau juhudi hizo za Serikali ya Tanzania katika kutimiza azma yake ya Maendeleo.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: