Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, January 6, 2022

Korea Kaskazini Yafanya Jaribio la kombora lenye kasi zaidi


Korea Kaskazini imesema  kwamba imefanikiwa kufyatua kombora liendalo kasi zaidi katika juhudi zake za kuimarisha mifumo yake ya kimkakati ya silaha siku chache baada ya kiongozi wake Kim Jong Un kuapa kuimarisha majeshi yake licha ya changamoto zilizosababishwa na janga la corona. 

Shirika kuu la habari la Korea Kaskazini limesema kamati kuu ya chama tawala imesema imeridhishwa sana na matokeo ya jaribio hilo la jana lililofuatiliwa kwa karibu na maafisa wandamizi ya masuala ya silaha.

 Jaribio hilo linaashiria kwamba taifa hilo litaendeleza mipango yake ya kuunda kombora la kisasa zaidi na wala halifikirii kurejea kwenye mazungumzo ya kuachana na mipango hiyo hivi karibuni.

 Hili ni jaribio la pili kwa taifa hilo kujaribu kombora linalokwenda kasi zaidi tangu jaribio la kwanza la Septemba mwaka jana.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: