Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, January 25, 2022

Majaliwa: Wazazi Shirikianeni Na Walimu Kukuza Taaluma


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wazazi wote washirikiane na walimu kuweka mazingira mazuri ya kitaaluma ili wahakikishe watoto wa Kitanzania wanapata elimu bora

Pia, Waziri Mkuu amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya wafuatilie katika maeneo yao ili kuona kama kuna shule zinaendelea kuchangisha michango ambayo iliyozuiliwa na Serikali.

Amesema hayo leo (Jumanne, Januari 25, 2022) alipokagua ujenzi wa madarasa ya shule ya Sekondari ya Babati Day iliyoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara.

“Wazazi lazima tushirikiane na walimu ili kuhakikisha watoto wote waliofikia umri wa kwenda shule wanakwenda na ni marufuku kuwakuta wakifanya biashara. Mtoto lazima asome.”

Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo, Lazaro Twange asimamie maboresho ya madawati katika shule hiyo kwa kuweka mbao badala ya mabati kama ilivyo sasa.

 “…Madawati haya si mazuri yarekebishwe ili kuepusha madhara kwa watoto wetu. Marekebisho haya yanatakiwa yafanyike bila kuathiri mwenendo wa masomo kwa wanafunzi.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaondoa hofu wananchi wote kuhusu gharama za kuunganishiwa umeme vijijini kwamba itaendelea kuwa sh. 27,000 tu.

Amesema wananchi hususan waishio vijijini hawahusiki na ongezeko la gharama za kuunganishiwa huduma ya umeme iliyotolewa hivi karibuni na Wizara ya Nishati.

Waziri Mkuu amesema malengo ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia ni kuhakikisha kuwa vijiji vyote vinapata umeme ifikapo Desemba mwaka huu.

Mheshimiwa Majaliwa amewataka wananchi hao waendelee kufanya maandalizi na malipo kwa ajili ya kuunganishiwa huduma hiyo katika makazi yao kwani ongezeko hilo haliwahusu.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amewahakikishia wananchi kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kusambaza huduma za maji.

Ameyasema hayo alipozungumza na wananchi katika kijiji cha Matufa baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Darakuta-Magugu utakaohudumia wananchi zaidi 80000.

Waziri Mkuu amesisitiza kwamba Serikali imedhamiria kufikisha huduma ya maji safi na salama katika maeneo yote nchini hadi vijiiini.”Endeleeni kuiamini Serikali yenu.”

Mradi huo una uwezo wa kuzalisha lita milioni 5.5 kwa siku, mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 95 na wananchi 45,000 wameanza kunufaika. Mradi huo umegharimu sh. bilioni 3.9.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, JANUARI 25, 2022.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: