Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, January 5, 2022

Marekani na EU waonya wanajeshi wa Sudan dhidi ya kumtaja Waziri Mkuu


Marekani, Norway, Uingereza na Umoja wa Ulaya zimeonya jeshi la Sudan dhidi ya kumteua waziri wao mkuu, zikisema kuwa hatua hiyo inaweza kulitumbukiza taifa hilo kwenye mzozo.

Nchi hizo zilisema hazitaunga mkono waziri mkuu au serikali iliyoteuliwa bila kushirikisha wadau mbalimbali wa kiraia.

Waziri mkuu wa zamani, Abdalla Hamdok, alijiuzulu siku ya Jumapili huku kukiwa na mkwamo wa kisiasa na maandamano makubwa yaliyotokana na mapinduzi ya kijeshi ya Oktoba.

Kwa mara nyingine tena nchi za Magharibi zimekemea hatua za jeshi dhidi ya waandamanaji - zaidi ya 50 wameuawa tangu mapinduzi.

Siku ya Jumanne, vikosi vya usalama vilirusha gesi ya kutoa machozi katika miji kadhaa kutawanya umati mkubwa wa watu waliokuwa wakiandamana kupinga utawala wa kijeshi

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: