Mkutano
wa 19 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na nchi za Nordic
unatarajiwa kufanyika mwezi Juni 2022 nchini Finland.
Hayo
yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) wakati alipokutana na kufanya
mazungumzo na Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan leo katika Ofisi
Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Katika
kuendeleza na kuimarisho ushirikiano wa nchi hizo mbili viongozi hao
wamependekeza kufanikisha ziara ya Mhe. Waziri Mulamula nchini Finland
pamoja na ushiriki wake katika mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje
wa Afrika Nordic utakaofanyika nchini Finland mwezi Juni 2022.
Katika
mazungumzo ya viongozi hao, Balozi Mulamula amemhakikishia Balozi Swan
kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana kwa karibu na Finland katika
kuhakikisha Mataifa hayo yanashirikiana kijamiii, kisiasa na kiuchumi.
“Finland
amekuwa mdau Mkubwa wa Maendeleo hapa nchini kwetu hasa katika sekta ya
fedha hususan katika masuala ya kodi, mazingira, tehama, uongozi pamoja
na uwezeshaji wa wanawake……..pia tumekubaliana kuendeleza ushirikiano
wetu kwa Maendeleo endelevu,” amesema Balozi Mulamula.
Katika
tukio jingine, Waziri Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Mtendaji
Mkuu wa Benki ya Stanbink Tanzania Bw. Kevin Wingfield
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )