Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, January 17, 2022

Mzee wa Miaka 57 Akamatwa Kwa Kuwabaka Mabinti Zake Watatu

JESHI la polisi mkoani Manyara linamshikilia mzee wa miaka 57 kwa tuhuma za kuwabaka watoto wake wa kike watatu, wenye umri wa miaka 15, 17 na 18.
 
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ilisema katika taarifa yake Jumatatu mshtakiwa yuko mahabusu. 
 
Kosa hilo lilifanyika wiki iliyopita, taarifa hiyo ilisema na kuongeza wasichana hao watatu kwa sasa wanaendelea na ushauri wa kisaikolojia.
 
Wizara iliwataka wananchi kufichua haraka matukio ya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili wa makundi yote kwa vyombo vya usalama vilivyo karibu ili kuzuia uharibifu zaidi kwa waathirika.
 
"Pia tunawaomba viongozi wa dini kutumia majukwaa yao kusaidia kueneza elimu itakayosaidia kukomesha unyanyasaji nyumbani," ilisoma sehemu ya taarifa hiyo iliyotiwa saini na mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini, Prudence Constantine.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: