Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, January 1, 2022

Nafasi 470 za Ajira Kutoka Idara ya Uhamiaji Tanzania


TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA ZA KONSTEBO WA UHAMIAJI (470)


Kamishna  Jenerali wa  Uhamiaji  anatangaza  nafasi  za ajira za  Konstebo wa  Uhamiaji 470 (Wenye  Shahada ya Kwanza nafasi  70, Kidato cha Sita  nafasi  100 na  Kidato cha Nne nafasi 300).
Waombajj  wawe wamefuzu  mafunzo mbalimbali ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) au Jeshi  la Kujenga Uchumi (JKU) waliopo Makambini au nje ya kambi wenye sifa zifuatazo:-


1.   SIFA ZA WAOMBAJI
i.      Awe raia wa Tanzania;
ii.     Awe na Cheti cha Kuzaliwa  (Birth Cetificate);
ii.     Awe na Kitambulisho au Namba ya Kitambulisho cha Taifa  (NIDA);
iv.     Awe  na vyeti  vya kuhitimu  shule  (Leaving   Certificates),  vyeti  vya taaluma
(Academic  Certificate)  na cheti  cha  kuhitimu  mafunzo  ya awali  ya JKT/JKU katika oparesheni mbalimbali;
v.      Awe na afya njema ya mwili na akili,
vi.      Awe  na tabia njema,  asiwe  amewahi  kufungwa,  kujihusisha  na  matumizi au biashara ya dawa za kulevya, au uhalifu wa aina yoyote;
vii.      Asiwe na alama yoyote au michoro  katika mwili wake;
viii.     Asiwe ameoa au kuolewa;
ix.     Awe tayari kuhudhuria  mafunzo ya awali ya Uhamiaji;
x.      Awe tayari  kufanya  kazi mahali popote nchini Tanzania;
xi.      Baada ya kuajiriwa  atafanya  kazi  kwa muda wa miaka  minne (4) bila kuoa au kuolewa;

xii.      Waombaji  wenye  Shahada  ya Kwanza wawe  na umri usiozidi miaka  30; awe amehitimu mafunzo katika moja ya fani zifuatazo:- Uhandisi  Ujenzi (Civil Engineering),   Umeme  (Electrical  Engeneering),   Mkadiriaji   Majenzi  (0S), Msanifu    Majengo   (Architect),   Afisa   Tabibu,    Tabibu   Msaidizi,    Uuguzi, Takwimu,   Masuala wa   Bima,   Msanifu Mifumo    ya  Kielekroniki   (System Developer),   Usalama wa  Mtandao (Cyber  Security),  Usalama  wa  Mifumo (Information  Security),  Wataalam   wa  Lugha  (Kiarabu,  Kichina,  Kifaransa, Kirusi,  Kihispaniola, Kitaliano,  Kireno), Wakalimani  (Translators) na  Mtaalam wa Lugha za alama;

xiii.    Waombaji  wa Kidato cha Sita na Nne wawe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi  miaka 28. 
Aidha,  waombaji  hao wawe na Cheti  cha Taaluma  kutoka katika Vyuo mbalimbali vinavyotambuliwa na serikali katika fani zifuatazo:• Umeme,    Ushonaji,   Ufundi   wa    Magari,    Fundi   Bomba,    Uashi,    Fundi Uchomeleaji,  Seremala,  Taaluma za  Uuguzi,  Mtunza kumbukumbu za Ofisi, Katibu   Muhtasi,   Tabibu,   Maabara,   Udereva,   Michezo,   Muziki,   Uimbaji, Uhandisi  wa Sauti (Sound Engineering),  Mpiga Vyombo vya Muziki,  Upishi,Ugani  pamoja  na  Fundi  wa Viyoyozi  (AC) - magari  au nyumba,  watapewa kipaumbele


2.  NAMNA YA KUTUMA MAOMBI:

Mwombaji anatakiwa  kuandika  barua ya Maombi ya ajira  kwa mkono wake akiambatisha  nyaraka  zifuatazo:•
i.    Barua ya Utambulisho toka Serikali ya Mtaa/Kijiji au Shehia;
ii.   Waombaji  waliopo  Makambini,  barua  zao zipitie  kwa Wakuu  wa Kambi husika;
iii.  Nakala ya Cheti cha Kuzaliwa;
iv.  Nakala  Kitambulisho  cha Taifa  (NIDA)  au  namba  ya  Kitambulisho  cha Taifa au Kitambulisho cha Mzanzibari;
v.   Nakala ya vyeti vya kuhitimu shule (Leaving  Certificates);
vi. Nakala ya vyeti vya Taaluma (Academic Certificates);
vii. Nakala ya vyeti vingine  vya Fani  mbalimbali;
viii.     Wasifu wa Mwombaji (CV);  na
ix.  Picha Nne (04) (Passport  size) zenye  rangi ya bluu bahari.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: