Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, January 4, 2022

Rais Samia ateua Wakurugenzi wawili na Katibu

 Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Dk Baghayo Abdallah Saqware kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA).

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Janueri 4, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu imesema kuwa Dk Saqware ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA).

Pia, mkuu huyo wa nchi amemteua Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania (Azania Bank Limited), Charles Jackson Itembe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Eneo Maalum la Mauzo ya Nje (EPZA).

Mwingine aliyeteuliwa na Rais Samia ni Ernest Maduhu Mchanga ambaye anakuwa Katibu wa Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC).

Kabila ya uteuzi huo, Mchanga alikuwa Katibu Msaidizi, Fedha na Utawala, Tume ya pamoja ya Fedha (JFC) kutoka Wizara ya Fedha na Mipango.

Taarifa hiyo imesema kuwa uteuzi wa viongozi hao umeanza Januari 1, 2021.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: