Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, January 7, 2022

Rais Samia: Vijana Msitumike Kupasua Chama


Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoruhusu watu wenye nia mbaya kuleta mpasuko na mgawanyiko ndani ya chama hicho.

Rais Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa ametoa wito huo wakati wa kilele cha matembezi ya miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibari huko wilaya ya mkoani Kusini Pemba.

Amesema kuna baadhi ya matukio ambapo Vijana ndani ya CCM wamekuwa wakitumiwa na watu hao wenye nia mbaya kuleta mpasuko na mgawanyiko ndani ya chama, jambo ambalo halipendezi.

Amewataka Vijana wa CCM kuwa mstari wa mbele kukitetea chama chao na kuwakemea wale wote wenye lengo la kuleta mpasuko na mgawanyiko.

Kaulimbiu ya matembezi hayo ya miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibari ni uchumi wa bluu ni fursa kubwa kwa Vijana.

Matembezi hayo yalizinduliwa tarehe tatu mwezi huu na kushirikisha watembeaji 700 waliotembea umbali wa kilomita 124.9 nchi nzima.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: