Tanzania na Jimbo la Dallas la nchini Marekani zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika nyanja za utalii, michezo, uwekezaji pamoja na kubadilishana uzoefu katika masuala ya uhifadhi wa maliasili pamoja na uendelezaji Utalii
Makubaliano hayo
yamefikiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro (Mb)
pamoja na viongozi mbalimbali katika Jimbo la Dallas wakati walipofanya
vikao vya ana kwa nyakati tofauti kwa lengo la kujifunza namna
wanavyoendesha shughuli za utalii pamoja kukuza ushirikiano baina ya
pande zote mbili
“Tumezungumzia
masuala ya kuimarisha uhusiano wetu baina ya Tanzania na Jimbo la
Dallas pamoja na kuangalia namna tunavyoweza kuliteka soko la watalii
katika Jimbo hilo, tumejadili mikakati ya kuanza na watalii ambao ni
wanafunzi wa vyuo vikuu katika jimbo hilo lengo likiwa ni kupata soko la
uhakika la watalii wengi zaidi katika siku za usoni ” Amesema Waziri
Ndumbaro
Akizungumza na Mkurugenzi wa
Idara ya Utalii wa Jimbo la Dallas Liliana Rivera, Dkt. Ndumbaro amesema
moja ya shabaha kubwa ni kuhakikisha kunaanzishwa ndege ya moja kwa
moja ya kutoka Tanzani kwenda Dallas ambapo amesema itaweza kusaidia
Watanzania ambao ni watalii kwenda Dallas na Watalii kutoka Dallas
kutembelea Tanzania
” Tanzania imeshaanzxa
mazungumzo na Uongozi wa Jimbo hilo ili kuhakikisha hilo linafanikiwa na
hivi wiki lijalo Mkurugenzi wa Shrika la Ndege Tanzania (ATCL) atakuja
Marekani kwa ajili ya kufanya mazungumzio hayo
Katika ziara hiyo
pia, Waziri Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais
wa Mchezo wa Gofu nchini Marekani, Bruce Davidson ambapo Dkt.Ndumbaro
ametumia fursa hiyo kuinadi Tanzania kuwa ipo tayari kuwa Mwenyeji wa
mashindano makubwa ya mchezo wa gofu yatayohusishwa Wachezaji mahiri
wa mchezo huo
“ Mchezo wa gofu ni
mchezo unaochezwa na watu wenye fedha nyingi hivyo kuwa wenyeji wa
mashindano hayo tutapata fursa ya. kutangaza vivutio vya utalii kwa
gharama nafuu kwa sababu wachezaji wakubwa pamoja na watu mashuhuri
watakuja Tanzania , kupitia umaarufu wao vyombo vikubwa vya habari
duniani vitaambatana nao kwa ajili ya kuripoti yatakayojiri” ameongeza
Waziri Ndumbaro
Aidha, Katika
mazungumzo hayo Dkt.Ndumbaro wamekubaliana kutangaza vivutio vya utalii
kupitia mchezo huo kwa kutumia vyombo vya habari vya kimataifa
vitakavyotumiwa katika kutangaza mchezom huo
Katika hatua
nyingine, Waziri Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na
Mkurugenzi Mtendaji wa Dallas Safari Club, Corey Mason ambapo katika
mazungumzo hayo wamezungumza maeneo ya kushirikiana ikiwemo kukuza
utalii wa uwindaji na kutoa vifaa vya kukabiliana na ujangili wa
wanyamapori
Aidha, Katika
mazungumzo hayo wamejadiliana masuala ya Uwekezaji ambapo Dkt.Ndumbaro
amewaita Wawekezaji wa Marekani hususan Matajiri wa Jimbo la Dallas
kuja kuwekeza Tanzani kwa kujenga mahoteli yenye hadhi ya nyota tano
Katika vikao hivyo
vya Waziri Ndumbaro aliambatana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani
nchini Marerkani Dkt. Elsie Kanza pamoja na Ujumbe wa kutoka Tanzania
akwemo Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA, Brigedia Jenerali, Hamisi Semfuko,
Mkurugenzi wa Wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha, Kaimu Kamishna Uhifadhi wa
TAWA, Mabula Misungwi na Afisa Mwandamizi, Segoline Tarimo
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )