Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, January 12, 2022

Urusi na China zapinga vikwazo dhidi ya Mali


Urusi na China zimeweka pingamizi, kuzuia azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililopendekeza vikwazo dhidi ya serikali ya kijeshi nchini Mali. 

Duru za kidiplomasia kutoka baraza hilo limesema mabalozi wa nchi hizo mbili wamelipinga pendekezo hilo lililokuwa limewasilishwa na Ufaransa. 

Wanajeshi walionyakuwa madaraka nchini Mali wameahirisha uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika mwezi Februari mwaka huu, na badala yake wametangaza kipindi cha mpito cha miaka hadi mitano, kuelekea mchakato wa kuipata serikali ya kiraia. 

Nchi za Afrika magharibi wanachama wa jumuiya ya kiuchumi ya ECOWAS, wameiwekea vikwazo vikali Mali, vinavyojumuisha kuifungia mipaka ya anga na nchi kavu, na vikwazo vya kibiashara. 

Mali imejibu kwa hasira hatua hizo, ikitishia kuondoka katika jumuiya hiyo.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: