Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, January 4, 2022

Wawili Wafariki Dunia Kwa Kugonga Gari Kwa Nyuma Magugu


Na John Walter-Babati
Watu wawili wamefariki dunia baada ya pikipiki waliyokuwa wamepanda kugonga lori kwa nyuma lililokuwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara kutokana na tairi kupata pancha.


Tukio hilo limetokea barabara kuu ya Arusha-Babati ambapo pikipiki yenye namba za usajili MC. 509 BDK iligongha gari hiyo yenye namba za Usajili T.336 AFE ambayo ni mali ya Siara Laizer.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Banjamin Kuzaga amewataja waliopoteza maisha kuwa ni Dereva wa pikipiki hiyo Daudi Jumanne (25) mkazi wa kijiji cha Magugu na Hussein Mustapha (21) mkazi wa kijiji cha Kiongozi tukio lililotokea Januari 2,2022 katika kijiji na kata ya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara.


Hata hivyo jeshi la polisi mkoa wa manyara linatoa wito kwa waendesha vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuzuilika.


Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: