Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, January 24, 2022

Waziri Ummy aagiza maduka ya dawa nje hospitali yaondolewe


Serikali imewaagiza wamiliki wa maduka ya dawa yaliyopo mita 500 kutoka vituo vya afya nchini kuyaondoa ifikapo Juni 30 mwaka huu.

Imeelezwa kuwa maduka hayo yapo kinyume cha kanuni ya famasia iliyowekwa mwaka 2020 hivyo wamiliki watachukuliwa hatua za kisheria.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu leo Januari 24, 2022 wakati wa ziara yake aliyoifanya katika hospitali ya Taifa Muhimbili-Upanga kwa lengo la kuangalia ubora wa utoaji huduma kwa wagonjwa.

“Ninatuma salamu maduka yote ya dawa lazima yawe mita 500 kutoka ndani ya hospitali, tunakwenda kuyaondoa ifikapo Julai Mosi mwaka huu tulishatoa muda wa kutosha kufikia Juni 30 yawe yameondoka.

“Wamiliki wanafanya kinyume cha sheria nipo na mfamasia Mkuu wa serikali hapa, tulitunga na tulipitisha kanuni maduka yote yawe mita 500 kutoka hospitalini nikaambiwa waziri kuna wengine walipewa leseni kabla, hivyo tumebakisha miezi mitano hakuna cha msalie mtume wala kuomba radhi,” amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy ameyasema hayo baada ya kukutana na malalamiko ya ukosefu wa dawa kutoka kwa wagonjwa hospitalini hapo.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: