Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, February 13, 2022

Dkt Mpango Azindua Sera Ya Taifa Ya Mazingira Ya Mwaka 2021 Jijini Dodoma


 Na Janeth Raphael - Dodoma
MAKAMU wa Rais Dkt. Philip Mpango ametoa siku 30 kwa Waziri wa Nchi,Muungano na Mazingira,Selemani Jafo na Waziri wa TAMISEMI kuandaa mpango mkakati wa kukijanisha na kusafisha Mji wa Dodoma.

Maagizo hayo ameyatoa  Februari 12,2022 jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa sera ya Taifa ya mazingira ya mwaka 2021 ambapo Makamu huyo wa Rais amelitaka Jiji la Dodoma kuandaa mpango huo lengo likiwa ni kuifanya Dodoma iwe ya kijani.

“Ninataka taarifa ya utekelezaji ya huo wa mpango mkakati kiuhalisia niupate kila baada ya miezi mitatu sasa kwenye hili pale utekelezaji utakapotokea unalega lega natoa tahadhari wahusika wote wawajibike wenyewe kabla sijaingilia kati natumaini wamenisikia.

“Hili zoezi liwe endelevu na nataka niupate mpango huu ndani ya miezi mitatu tunataka Dodoma iwe kama Singapore lazima Dodoma iwe ya kijani lazima Dodoma iwe safi,”amesema.

Dk.Mpango amesema kuwa katika ziara zake zote atakazofanya , ajenda yake ya kwanza katika Mkoa husika itakuwa ni ujanishaji, upendezeshaji na usafi wa mazingira wa mahali hapo!

Dkt Mpango ameitaka NEMC, kuhakikisha wanalinda na kuhifadhi vyanzo vya maji hususan katika mito na maeneo oevu nchini yasiendelee kuharibiwa.

”Kwa mfano, kwenye chanzo cha mto Ruaha katika Bonde la Ihefu, Mbeya, hakikisheni kuna matumizi endelevu ya mto huo pamoja na mito mingine nchini.”amesema Dk.Mpango

Aidha amewataka Mawaziri wa Waziri wa Ardhi, Waziri wa Maji, Waziri wa Kilimo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara na Mazingira kwenda kufanya tathmini na kumpa majibu hatua walizochukua katika ujenzi wa bwawa la mwalimu Nyerere.

”Sitakuwa tayari kama Makamu wa Rais kuona tunakamilisha ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere halafu baadae maji hayapatikani kutokana na uharibifu unaofanyika katika vyanzo vya mto Rufiji, tunafahamu kuwa shughuli za kilimo na mifugo ni muhimu katika ukuaji wa uchumi wetu lakini zifanywe bila kuvunja sheria za uhifadhi wa mazingira.”amesisitiza

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,Selemani Jafo amesema awali kulikuwa na sera ya mwaka 1997 ambayo ilipata mafanikio makubwa na kuzalisha sheria namba 20 ya mwaka 2004 na kanuni zake.

Amesema kwa kuwa Sasa kwa sasa kuna mahitaji makubwa na matakwa mbalimbali ilisababisha waunde sera mpya ya mazingiraa ambayo imezinduliwa leo.

Amesema Juni 5 mwaka 2021,wakati Makamu wa Rais akizindua kampeni kapambe ya mazingira alitoa maelekezo ambayo ni pamoja na kuhakikisha sera ya mazingira inakamilika.

Amesema kwa kupitia sera hiyo Tanzania inaenda kuwa sehemu salama katika suala la mazingira na kuungana na mataifa mengine.

“Sera hii itaenda kuongeza fursa za jinsi gani urejeshaji wa taka unaweza kujenga uchumi wa mtu mmoja mmoja ama vikundi mbalimbali hili ni jambo ambalo lipo katika sera yetu jinsi gani tutatumia mbinu mbadala taka zinarejeshwa,”amesema.

Amesema sera hiyo itaenda kuakisi hasa mabadiliko ya tabia nchi ambapo amemhakikishia Makamu wa Rais kwamba imezingatia Mpango wa Taifa wa miaka mitano 2020-21mpaka 2025-2026 mpango endelevu wa mwaka 2030 na mpango ule wa miaka 15 ulioanza mwaka 2011-2012 mpaka 2025-2026.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: