Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, February 11, 2022

Joe Biden awataka raia wa Marekani kuondoka Ukraine mara moja


Rais wa Marekani Joe Biden ametoa wito kwa raia wote wa Marekani waliosalia nchini Ukraine kuondoka nchini humo mara moja kutokana na kuongezeka kwa vitisho vya kuchukuliwa hatua za kijeshi za Urusi.

Biden alisema hatatuma wanajeshi kuwaokoa Wamarekani ikiwa Moscow itavamia Ukraine.Alionya kwamba "mambo yanaweza kutokea haraka" katika eneo hilo.

Urusi imekanusha mara kwa mara mpango wowote wa kuivamia Ukraine licha ya kuwa na wanajeshi zaidi ya 100,000 kwenye mpaka.

Lakini ndiyo kwanza imeanza mazoezi makubwa ya kijeshi na nchi jirani ya Belarus, na Ukraine imeishutumu Urusi kwa kuizuia kuingia baharini.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson alisema Alhamisi kwamba Ulaya inakabiliwa na mzozo mkubwa zaidi wa usalama katika miongo kadhaa huku kukiwa na mvutano.

-BBC

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: