Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, March 21, 2022

Mtoto aliyewadhalilisha wenzake kufikishwa mahakamani


Kesi nane za ukatili wa kingono kati ya 19 zinazohusu watoto waliodhalilishwa na mtoto mwenzao mwenye umri wa miaka 14 mkoani Iringa, zinatarajiwa kufikishwa mahakamani wiki hii.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa, Allan Bulumbi amesema kuwa uchunguzi wa daktari umebaini kuwa watoto wote wamedhalilishwa na mtoto huyo ambaye anashikiliwa na polisi kulinda usalama wake.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwapatia zawadi za pipi, pesa na kuwaruhusu kuangalia televisheni nyumbani kwao, ili wakubali udhalilishaji huo.

Matukio ya ukatili wa kingono mkoani Iringa yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku, ambapo mwaka 2021 pekee watoto 384 walifanyiwa ukatili wa aina hiyo.

Wadau wa kupinga ukatili mkoani humo wamewataka wazazi kuchukua nafasi yao ya malezi ili kuwanusuru watoto na ukatili wa kingono.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: