Serikali ya
Tanzania imewakaribisha wawekezaji wa masuala ya kilimo kuwekeza nchini
ili kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo na kuimarisha lishe
kwa wananchi na kuinua pato la Taifa.
Kauli hiyo
imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, na Uratibu
Mhe. Balozi. Dkt Pindi Chana alipokutana na kufanya mazungumzo na
Mwakilishi wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) Tanzania Bi.
Sarah Gibson na Mkurugenzi wa Shirika hilo Kanda ya Kusini wa Afrika
Dkt. Manghestab Haile Ofsini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Akileleza baadhi
ya masuala yaliyoafikiwa ni pamoja na kuboresha suala la lishe kwa
wananchi licha ya uzalishaji mkubwa wa chakula katika maeneo mbalimbali
hatua itakayoboresha afya na kuepuka utapiamlo huku akisema kuwa
Tanzania ni sehemu salama kwa ajili ya kufanya uwekezaji katika nyanja
ya kilimo.
“Tunaposhirikiana
na WFP chini ya Rais wetu mpendwa Mhe. Samia Suluhu Hassan Tanzania ni
eneo sahihi kabisa katika uzalishaji wa chakula tumekuwa tukizalisha
chakula cha kutosha na tumekuwa mfano ndani ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Nchi za SADC na
tumekuwa tukipeleka chakula nje ya Nchi,”alisema Mhe. Pindi Chana.
Pia Waziri Pindi
alieleza kwamba wamefikia makubaliano ya kushirikiana katika masuala ya
maafa pindi yanapojitokeza kwani yamekuwa yakisababisha maafa kwa raia
kama vifo, mali zao kuharibiwa na miundo mbinu.
Vilevile Mhe.
Pindi alibainisha kwamba wamekubaliana kuboresha sula la kilimo kuendana
na teknolojia iliyopo sasa na matumizi sahihi ya pembejeo pamoja na
ushirikishwaji wa vijana katika uzalishaji wa chakula, masoko na
kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo.
“Katika
majadiliano tumezungumzia suala zina la kilimo kuna matumizi ya vitendea
kazi vya kisasa, ushirikishwaji wa vijana maana idadi kubwa ya umri wa
watu ni vijana na sasa tunaelekea sensa ya watu na makazi mwaka huu
asilimia 50 kwahiyo ni jinsi gani tunahamasisha vijana katika
uzalishaji wa chakula na kuongeza thamani yake,” alieleza Mhe. Pindi.
Katika hatua
nyingine aliwahakikisha kwamba kuelekea Bunge la bajeti ijayo sekta ya
kilimo imepewa kipaumbele kuhakikisha kinaleta tija na kuona namna ya
kushrikiana na WFP kuboresha eneo hilo muhimu la chakula.
Kwa upande wake
Mwakilishi wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa nchini Tanzania (
WFP) Bi. Sarah Gibson aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa namna
ambavyo imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Taifa linakuwa na chakula
cha kutosha na chenye ubora akisisitiza kuendeleza uhusiano baina
Tanzania na Shirika hilo.
Naye Mkurugenzi
wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) wa Kanda ya Kusini mwa
Afrika Dkt. Manghestab Haile aliiahidi Serikali ya Tanzania kuendelea
kushirikiana na sekta binafsi, kuimarisha masoko na lishe bora kwa raia
wake.
Akihitimisha
Mkurugenzi Msaidizi wa Menejimenti ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu
Bw.Charles Msangi alishukuru ugeni huo wa wadau wa maendeleo na kusema
kwamba utasaidia kutatua changamoto zilizopo katika usimamizi wa maafa.
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )