Naibu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Bw. Xavier Daudi amesema, tangu kuanzishwa kwa mfumo wa
kielektroniki wa kupokea, kufuatilia na kushughulikia malalamiko
(e-Mrejesho) kumekuwa na mwitikio chanya wa wananchi na watumishi wa
umma kuutumia mfumo huo, ambao umeiwezesha Serikali kupokea na
kushughulikia kwa wakati jumla ya maoni na malalamiko 239,196
yaliyowasilishwa katika Taasisi za Umma.
Bw.
Daudi amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo ya
matumizi na uendeshaji wa mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia
malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi (e-Mrejesho) kwa Maafisa
Malalamiko na TEHAMA wa Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za
Mitaa, Wizara, Wakala na Idara Zinazojitegemea ambao wamepewa dhamana ya
kushughulikia malalamiko kwenye taasisi zilizopo Kanda ya Mashariki.
Bw.
Daudi amesema kuwa, miaka ya nyuma kabla ya kuanzishwa kwa mfumo huo wa
kielektroniki haikuwa rahisi kushughulikia malalamiko kwa wakati na
kuwa na takwimu halisi za maoni na malalamiko yaliyofanyiwa kazi ambazo
zinatumiwa na Serikali kama mrejesho wa kuboresha huduma zinazotolewa na
Taasisi za Umma kwa wananchi.
Aidha,
Bw. Daudi ameeleza kuwa, Ofisi ya Rais – UTUMISHI kupitia Idara ya
Ukuzaji Maadili imejipanga kuendelea kutoa mafunzo kwa Maafisa
Malalamiko na TEHAMA katika taasisi zote za umma nchini, ili kuwajengea
uwezo wa kutumia vema mfumo huo wa kieletroniki kushughulikia malalamiko
yote yanayowasilishwa na wananchi na wadau kwa wakati.
Bw.
Daudi ameongeza kuwa, Mfumo wa e-Mrejesho umesanifiwa kwa namna ambayo
inaongeza uwazi, uwajibikaji na usikivu kwa watendaji Serikalini, kwani
mfumo unawawezesha viongozi katika ngazi mbalimbali kuona na kufuatilia
namna ambavyo malalamiko au maoni yanavyoshughulikiwa.
“Endapo
kutakuwa na ucheleweshwaji wa kutoa mrejesho au uzembe wa aina yoyote,
mfumo unampa fursa kiongozi katika taasisi husika kuchukua hatua stahiki
kwa wakati,” Bw. Daudi amefafanua.
Sanjari
na hilo, Bw. Daudi amesema kuwa, mfumo huo ni rahisi kuutumia kwa kuwa
unamuwezesha mtumishi na mwananchi wakati wote na popote alipo kutuma
maoni au malalamiko na kupokea mrejesho kupitia tovuti au simu za
kiganjani.
Akisisitiza
suala la uwajibikaji, Bw. Daudi ametoa rai kwa washiriki wa mafunzo
hayo, kuhakikisha wanaratibu ushughulikiaji wa malalamiko kwa wakati ili
mfumo huo uwe na tija kwa wananchi na manufaa kwa Serikali katika
kuboresha huduma inazozitoa kwa wananchi.
Akitoa
neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu kuzungumza
na washiriki wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Idara ya Ukuzaji Maadili, Ofisi
ya Rais – UTUMISHI, Bi. Leila Mavika amesema kuwa, njia ambazo zilikuwa
zikitumika kuwasilisha malalamiko hapo awali zilisababisha changamoto
mbalimbali ikiwemo ya kukosekana kwa takwimu sahihi za utunzaji wa
takwimu za malalamiko ambazo hutumiwa na Serikali kuboresha huduma na
kufanya maamuzi.
Bi.
Mavika ameeleza kuwa, kabla ya Serikali kuanzisha mfumo wa
kushughulikia malalamiko kielektroniki, wananchi hawakuwa na fursa ya
kupata mrejesho wa malalamiko yao kwa wakati hivyo Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kushirikiana na
Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) iliona ni vema kuandaa mfumo wa
kielektroniki ambao kwa kiasi kikubwa utaongeza uwajibikaji katika eneo
la kushughulikia malalamiko.
Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia Idara
yake ya Ukuzaji wa Maadili na Idara ya Mifumo ya TEHAMA inatoa mafunzo
ya kutumia mfumo wa e-Mrejesho kwa Maafisa Malalamiko na TEHAMA katika
Taasisi za Umma ziliozopo mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara,
yanayofanyika jijini Dar es Salaam kwa siku nne (4) katika Ukumbi wa
Chuo cha Kodi.
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )