Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, March 11, 2022

Wakuu wa idara matatani kwa kukiuka taratibu za manunuzi


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) Innocent Bashungwa amemuagiza Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro kuwachukulia hatua za kiutumishi wakuu wa Idara wote wa halmashauri ya wilaya ya Mvomero waliohusika na ukiukwaji wa taratibu za manunuzi kwenye ujenzi wa shule ya Sokoine Memorial High School.

Akizungumza na viongozi wa mkoa wa Morogoro pamoja na wale wa halmashauri ya wilaya ya Mvomero wakati akikagua miradi inayotekelezwa katika halmashauri hiyo Waziri Bashungwa amesema kuwa, kumekuwa na dosari kwenye manunuzi ndani ya halmashauri ya wilaya ya Mvomero.

Amesema Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika halmashauri ya wilaya ya Mvomero, lakini kumekuwa na dosari katika manunuzi, jambo linalosababisha miradi kukwama na kutomalizika kwa wakati.

Aidha, amewaagiza Wakurugenzi wote nchini kufuata sheria, kanuni na taratibu za manunuzi katika kuendesha halmashauri ili wasiingie kwenye matatizo ambayo yanatokana na kwenda kinyume na utaratibu

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: