Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, March 4, 2022

Wanafunzi wa Kitanzania Ukraine waruhusiwa kuvuka mpaka wa Urusi


Wanafunzi wa Kitanzania walio katika mji wa Sumy nchini Ukraine wameruhusiwa kutoka nchini humo kupitia mpaka wa Russia baada ya mazungumzo ya kidiplomasia kufanyika na Serikali ya Russia kuridhia.

Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa leo Machi 4, 2022  na Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden na Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi, shughuli ya kuwatoa wanafunzi wote kutoka Sumy hadi kwenye mpaka wa Russia, litaratibiwa na Serikali hiyo na tayari imeanza mipango ya utekelezaji.

“Wanafunzi hao watakapofika mpakani, Ubalozi wa Tanzania nchini Russia utawapokea kwa taratibu nyingine za kurejea nyumbani,” inaeleza taarifa hiyo ya Balozi hizo.

Taarifa hiyo inaeleza kwamba wakati shughuli ya kuwatoa wanafunzi walioko Sumy ikiendelea  kuratibiwa, Balozi zinaomba wanafunzi hao pamoja na wazazi kuwa wavumilivu ili kuhakikisha wanatoka kwa usalama nchini Ukraine.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: