Na Mathias Canal, Dar es salaam
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof. Adolf Mkenda ameteua kamati ya mpito ya watu watatu ambayo itashughulikia shughuli za kiutendaji za Scauti Tanzania.
Kamati hiyo tendaji pia imepewa jukumu la kuhakikisha inaandaa Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa uongozi wa Scauti.
Ameitaka kamati hiyo ya mpito kuhakikisha kuwa inatoa Notisi tarehe 21 Machi 2022 na kuagiza mkutano mkuu ufanyike ndani ya siku 21 mara baada ya tangazo hilo.
Waziri Mkenda ametoa agizo hilo leo tarehe 18 Machi 2022 wakati wa kikao kazi na kamati tendaji ya Scauti Tanzania akiwa ameambatana na Scauti Mkuu Tanzania Bi Mwantumu Maiza kilichofanyika Ofisini kwake Jijini Dar es salaam
Waziri Prof Mkenda amesema kuwa kamati hiyo tendaji itaongozwa na Bw Stewart Kiluswa akisaidiana na Omary Mavura pamoja na Suleiman Takadiri