Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, April 25, 2022

Kinana Awataka Wabunge Na Madiwani Kutopitisha Sheria Zinazominya Haki Na Kuwabana Wananchi


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amewataka  madiwani na wabunge kukataa  kupitisha  miswada ya Sheria  yenye kukandamiza haki na kuminya fursa ya wananchi wanyonge kujiendeleza kiuchumi.

Pia, amesema Sasa ni wakati muafaka  kulitazama vyema  kundi la wajasiriamali wadogo wakiwemo mamalishe na bodaboda ili wawekewe mazingira mazuri ya kunufaika na juhudi zao.

Kinana ameyasema hayo leo mjini Korogwe, wakati akizungumza na wana CCM katika ukumbi wa Lembeni, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na kujitambulisha kwa wanachama.

"Madiwani nyinyi ndio mnaosimamia sheria za Halmashauri, mkiona sheria hazina uhusiano na wananchi kataeni. Mkiletewa sheria pelekeni kwa wananchi waulizeni, rahisisheni maisha ya watu muwasidie wakue.

"Wabunge wa Bungee la Jamhuri ya Muungano...sheria ikija bungeni waambieni (serikali) kwa sasa hatuipitishi mpaka tukashauriane  na wananchi," alisema.Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: