Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, May 28, 2022

Tangazo la Ajira Mpya 104 Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali


Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi mia moja na nne (104) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.

1.0 OFISI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI (NAOT)
Ibara ya 143 inampa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jukumu la kudhibiti fedha zote zinazotoka katika Mfuko Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kufanya ukaguzi wa mapato na matumizi ya rasilimali za umma kama zinavyoidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vile vile, Ibara ya 143 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali baada ya kufanya ukaguzi huo wa mapato na matumizi angalau mara moja kila mwaka, anatakiwa kuwasilisha Taarifa ya ukaguzi kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya tarehe 31 Machi, na Mheshimiwa Rais ndani ya siku saba (7) ataelekeza Mawaziri wanaohusika kuwasilisha taarifa hizo Bungeni.

Aidha, katika kuhakikisha kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anatekeleza ipasavyo jukumu hilo la Kikatiba, Kifungu cha 20 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma, Sura 418 kimeanzisha Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ambayo inaongozwa na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali. Kwa mujibu wa Kifungu hicho, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kwa niaba ya Bunge, atachunguza, atahoji na kukagua hesabu zinazowasilishwa kwake kama ilivyoelekezwa chini ya Sheria ya Fedha za Umma, Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa na Sheria nyingine yoyote, na kutekeleza majukumu mengine yoyote ambayo ameidhinishwa kutekeleza na au chini ya Sheria tajwa.

Vile vile, Sehemu ya Nne ya Sheria ya Ukaguzi wa Umma, inamtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kupitia Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kufanya aina mbalimbali za ukaguzi ikiwemo ukaguzi wa hesabu; ukaguzi wa uzingatiaji sheria; ukaguzi wa ufanisi; ukaguzi wa kiufundi; ukaguzi wa kiuchunguzi; na ukaguzi wa Mifumo ya TEHAMA.

==>>BOFYA HAPA KUZAMA NAFASI 104 NA KUTUMA MAOMBI

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: