China na Urusi zimetumia kura za turufu kupinga azimio la Umoja wa
Mataifa juu ya kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini. Azimio hilo lilikuwa na
lengo la kuiwekea nchi hiyo vikwazo vipya vikali zaidi baada ya kufanya
majaribio kadhaa ya makombora ya masafa marefu yanayoweza kubeba mabomu
ya nyuklia. Wajumbe 13 walipiga kura kuliunga mkono azimio hilo.
Urusi
na China zimesema zinapinga vikwazo zaidi na zimesisitiza kuwa
kinachohitajika sasa ni mazungumzo mengine baina ya Korea Kaskazini na
Marekani.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliweka vikwazo dhidi
ya Korea Kaskazini mnamo mwaka 2006 baada ya nchi hiyo kufanya jaribio
la kwanza la silaha za nyuklia.
Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa
Mataifa Linda Thomas-Greenfield ameelezea masikitiko yake juu ya kura za
China na Urusi na amesema majaribio ya makombora ya masafa marefu
yaliyofanywa na Korea Kaskazini mnamo mwaka huu ni tishio kubwa kwa
usalama wa dunia.
Tangazo
ap
taboola dsk
ad
Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )