Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, May 25, 2022

China, Urusi zarusha ndege za kivita karibu na Japan


China na Urusi zimerusha ndege zao za kivita karibu na bahari ya Japan katika kile Marekani inachosema ni ishara ya uhusiano usio mipaka kati ya Beijing na Moscow. 

Wizara ya Ulinzi ya China imethibitisha kwamba ilifanya "doria ya pamoja ya kimkakati" kwenye Bahari ya Japan, Bahari ya Mashariki ya China na Bahari ya Pasifiki kwa mujibu wa mpango wa kila mwaka wa ushirikiano wa kijeshi kati yake na Urusi. 

Waziri wa Ulinzi wa Japan, Nobuo Kishi, amesema kuwa ndege hizo ziliruka siku nzima ya jana na kwamba hatua hiyo ilikuwa ni "tendo la ishara" wakati mkutano wa Quad ukiendelea mjini Tokyo, kati ya rais wa Marekani na mawaziri wakuu wa Japan, Australia na India.

 Korea Kusini imesema pia kuwa ndege hizo za Urusi na China ziliingia kwenye eneo lake la ulinzi wa anga, ingawa hazikuingilia mamlaka yake ya anga.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: