Uturuki imesema itapinga mpango wa Sweden na Finland wa kutaka
kujiunga kwenye mfungamano wa kijeshi wa NATO. Rais wa Uturuki Recep
Tayyip Erdogan amesema kwamba amewaambia washirika wa NATO kwamba
Uturuki inapinga hatua ya kujiunga kwa nchi hizo mbili.
Erdogan amesema
pingamizi la Uturuki linatokana na matatizo yaliyopo kati ya nchi yake
na Sweden na Finland ambapo Uturuki inazilaumu nchi hizo kwa kuwapa
hifadhi wafuasi wa Fethullah Gulen, kiongozi wa dini ya Kiislamu mwenye
makazi yake nchini Marekani ambaye Uturuki inamlaumu kwa kuhusika na
jaribio la mapinduzi la mwaka 2016.
Uturuki imesema inazitaka Finland na
Sweden ziache kuwapa misaada Wakurdi wanaoipinga Uturuki na pia ziondoe
vikwazo vya silaha walivyoweka dhidi ya nchi hiyo.
Tangazo
ap
taboola dsk
ad
Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )