Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, May 27, 2022

Serikali yatangaza kiwango kipya cha kikotoo


 Serikali imetangaza kiwango kipya cha kikotoo cha mafao ya mkupuo ambapo sasa ni asilimia 33 kwa mifuko yote ya hifadhi ya jamii.

Tangazo hilo la Serikali limetolewa jijini Dodoma na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu Profesa Jamal Katundu.

Amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya makubaliano kati ya Serikali, Chama cha Waajiri Nchini (ATE) na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) baada ya kusitishwa kwa kanuni zilizotengenezwa mwaka 2018.

Profesa Katundu amesema wamekubaliana kikokotoo limbikizi kitakuwa 1/580.

Amesema mshahara wa kukotolea mafao ya pensheni utakuwa wastani wa mishahara bora ya miaka mitatu ndani ya miaka 10 kabla ya kustaafu.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: