Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema leo zaidi ya wanajeshi 900 wa
Ukraine wamejisalimisha katika kiwanda cha chuma cha Azovstal mjini
Mariupol. Katika taarifa yake ya kila siku kuhusiana na mzozo huo,
wizara hiyo imesema jumla ya wanajeshi 959 wamejisalimisha tangu Mei 16,
80 kati yao wakiwa wamejeruhiwa.
Wizara hiyo imesema wale wanaohitaji
matibabu wamepelekwa katika hospitali moja iliyoko mji wa Novoazovsk
unaodhibitiwa na Urusi.
Ukraine inatarajia kuwabadilisha wafungwa wa
Urusi na wanajeshi hao waliojisalimisha ila Urusi haijathibitisha iwapo
hilo litafanyika.
Mwezi uliopita, Urusi ilidai kuchukua udhibiti wa
Mariupol baada ya wiki kadhaa za mashambulizi, ila mamia ya wanajeshi wa
Ukraine walikuwa wamejificha katika mahandaki ya chini ya ardhi kwenye
kiwanda hicho cha Azovstal.
Wizara ya ulinzi ya Ukraine inasema itafanya
kila iwezalo kuwanusuru wapiganaji waliosalia kiwandani humo ambao
idadi yao haijulikani kwa sasa, ila ikadai hawatofanya operesheni ya
kijeshi.
Tangazo
ap
taboola dsk
ad
Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )