Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, May 17, 2022

Wakurugenzi watano MSD waondolewa


Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametangaza kuondolewa kazini Wakurugenzi watano wa Bohari ya Dawa (MSD), kufuatilia malalamiko mengi ambayo yamekuwa yakitolewa na wabunge na wadau wengine kuhusu utendaji usioridhisha wa bohari hiyo.

Waziri Ummy Mwalimu ameliambia bunge jijini Dodoma kuwa pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan kubadilisha uongozi wa juu wa MSD na kumteua mwenyekiti mpya wa bodi, hatua hiyo ilikuwa haitoshi kutokana na malalamiko mengi yaliyokuwa yakitolewa.

“Mkurugenzi wa Fedha anaondoka MSD, Mkurugenzi wa manunuzi MSD, Mkurugenzi wa Logistics MSD, Mkurugenzi wa Sheria MSD na Mkurugenzi wa Utawala wa MSD anaondoka.” amesema Waziri Ummy Mwalimu

Waziri huyo wa Afya ametangaza uamuzi huo wakati akihitimisha mjadala wa bajeti kwa wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023, baada ya kuchangiwa na wabunge mbalimbali.

Pia amesema wizara ya afya itasimamia ubora na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba na kuipima MSD kwa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa miezi mitatu mitatu badala ya mwezi mmoja mmoja

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: