Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, June 16, 2022

Atiwa Mbaroni Kwa Kujifanya Mkuu Wa Mkoa Wa Mbeya.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia WARREN MAX MWINUKA [20] Mkazi wa Makondeko – Mbeya Mjini kwa tuhuma za kujifanya Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya JUMA ZUBERI HOMERA akitumia akaunti ya mtandao wa kijamii wa Instagram kwa jina la “juma_homera”.

Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 07.06.2022 majira ya saa 08:00 mchana huko maeneo ya Mama John Jijini Mbeya. Mtuhumiwa alikuwa akitumia akaunti hiyo kuwaadaa watu kwa kujifanya ni Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na kutoa namba ya simu yak wake ili wananchi waweze kutoa/kupeleka kero/shida mbalimbali kwake. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika atafikishwa mahakamani.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: