CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeiomba Serikali kuangalia namna bora ya kufufua na kukwamua mchakato wa Katiba mpya kwa maslahi mapana ya Taifa.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya CCM itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka
ameyasema hayo Juni 22,2022 jijini Dodoma wakati akizungumza na
waandishi wa habari.
Shaka
amesema, katika kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu walichokaa
wamekubaliana suala la Katiba mpya liangaliwe kwa maslahi mapana ya
Taifa.
Amesema,Halmashauri
Kuu ya Taifa kwa kauli moja imekubaliana upatikanaji wa Katiba mpya na
chama hicho kinakubaliana na umuhimu wa kupatikana izingatie mazingira
ya sasa.
Pia
akizungumzia masuala ya Uchaguzi Mkuu wa ndani ya chama,Shaka amesema
Halmashauri Kuu ya Taifa imepokea na kuridhishwa taarifa ya maendeleo ya
uchaguzi wa ndani ya chama ambao umeshakamilika kwa asilimia 99.5
katika ngazi ya mashina na matawi kote nchini na sasa upo katika ngazi
ya kata na wadi.
Pia
amesema kuwa, miongoni mwa mambo ambayo Halmashauri Kuu imeshauri
kutazamwa ni pamoja na kesi zenye sura ya kisiasa kwa wafuasi na
wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa nchini.
Amesema,
chama kimeishauri Serikali utekelezaji wa masuala yote ya kuimarisha
demokrasia nchini na kutaka mazingira ya kisiasa yafanyike bila kuathiri
uhuru na usalama wa nchi yetu.
Licha
ya hayo ameeleza kuwa Halmashauri Kuu ya Taifa imempongeza Rais Samia
Suluhu Hassan kwa ukomavu, ustahimilivu, uhodari na dhamira yake njema
ya kufanya maridhiano na vyama vya siasa nchini kwa lengo la kuimarisha
umoja, ushirikiano, mshikamano, amani na utulivu kwa maendeleo na ustawi
wa watanzania wote.
"Halmashauri
Kuu ya Taifa imevipongeza vyama vyote vya siasa kwa kukubali kuunga
mkono hatua hiyo, chama kimeishauri Serikali kuharakisha utekelezaji wa
masuala yote yatakayojenga kuaminiana, kuimarisha ushirikiano na umoja
wa kitaifa kwa ustawi wa wananchi wote,"amesema.
Vilevile
Halmashauri Kuu ya Taifa imempongeza Rais wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Husein Ali Mwinyi kwa
kuendelea kuonesha uvumilivu na ukomavu wa kiuongozi katika kuongoza
serikali ya umoja wa kitaifa, hali inayochochea umoja, amani na utulivu
kwa wananchi wa Zanzibar na hivyo kuharakisha maendeleo yao.
Hayo
yanajiri baada ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
kuongoza Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
iliyokutana leo Juni 22, 2022 katika Ukumbi wa White House makao makuu
ya CCM jijini Dodoma ikiwa ni utaratibu wa vikao vyake vya Kitaifa.
Juni
21,2022 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM) iikutana Ikulu Chamwino, Dodoma kwa kikao cha siku moja cha
kawaida na kufuatia kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kilichofanya
uchaguzi wa kujaza nafasi mbili za wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri
ya Taifa zilizokuwa wazi kwa kuwachagua kwa kura Stephen Masatu Wassira
na Theresia Adriano Mtewele.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa,Itikadi na Uenezi (NEC) Shaka Hamdu Shaka
amesema, vikao hivyo vyote viwili vimejadili masuala mbalimbali ya
msingi na kwamba pamoja na mambo mengine, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu
ya Taifa ya CCM imefanya uteuzi wa wenyeviti wa halmashauri za wilaya na
mameya.
Shaka
amesema, uteuzi huo ni Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Mji,Erasto B.
Mpete,Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro,Mohamed Festo Bayo na
Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Stuart Nathaniel Nkinda, Apaikunda Ayo
Naburi na Zuberi Abdallah Kidumo.
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )