Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, June 15, 2022

Mtanzania kuanzia miaka 18 kuanza kulipa kodi


Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema Serikali inakusudia kutoa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kila Mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 kuanza kulipa kodi.

Dk Mwigulu amebainisha hayo  Jumanne Juni 14, 2022 bungeni jijini Dodoma, wakati akiwasilisha mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2022/23.

Waziri huyo amesema ili kufikia azma hiyo wataanza kutoa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kila mtanzania  kuanzia umri wa kuanzia miaka 18 kwa utaratibu wa usajili wa namba ya utambulisho wa Taifa (NIDA) unaomtaka kila mwananchi mwenye umri huo wa au zaidi kujisajili.

“Napendekeza kuwa wale wote wenye NIDA kwa sasa (wanaofikia milioni 19 nchi nzima) wapatiwe namba ya TIN na itumike kwenye miamala yote inayofanyika katika ununuzi na mauzo yanayofanyika ndani ya nchi,”amesema

Waziri huyo amefafanua kuwa kila mwenye namba ya mlipakodi atapata makadirio yake kwa njia ya simu na kulipa kodi husika kwa njia ya mtandao.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: