Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, June 10, 2022

Profesa Jay aruhusiwa kutoka hospitali

Mkongwe wa Hiphop na mbunge wa zamani wa Mikumi, Joseph Haule maarufu kwa jina la Profesa Jay, jana ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kulazwa kwa siku 127 akifanyiwa matibabu.

Profesa Jay alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam akipatiwa matibabu ya figo tangu Februari Mosi, 2022.

Taarifa iliyotolewa leo Juni 10, 2022 na hospitali hiyo imeeleza kuwa mwanamuziki huyo alipatiwa matibabu kwa takribani siku 127 na sasa ameruhusiwa kurejea nyumbani baada ya afya yake kuimarika.

“Msanii Joseph Haule (Prof. J) jana ameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupatiwa matibabu kwa siku 127 na afya yake kuimarika” imeeleza taarifa hiyo.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: