SERIKALI
imesema katika kuboresha sekta ya kilimo ikiwemo kuongeza mnyororo wa
thamani imeongeza bajeti yake mara mbili zaidi kutoka Sh bilioni 228
hadi Sh bilioni 751 mwaka 2022/23.
Kauli
hiyo imetolewa mkoani Arusha na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo,Gerald Mweli,kwa niaba ya Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, katika
mkutano wa wadau wa mbegu hapa nchini, ulioandaliwa na Kituo cha utafiti
cha Kimataifa cha World Vegetable Centre kwa kushirikiana na Ubalozi
wa Uholanzi nchini Tanzania.
Alisema
miongoni mwa vipaumbele vyake ni pamoja na kuboresha uzalishaji na
usambazaji wa mbegu ambapo imetenga Sh bilioni 300 kwa ajili ya skimu za
umwagiliaji.
Naibu
huyo alisema kuendelea kuimarisha tafiti kwa ajili ya upatikanaji wa
mbegu bora, uwepo wa masoko utasaidia kupunguza vikwazo kwenye sekta
hiyo na kuwa kikao hicho ni alama kwamba wadau na washirika wa maendeleo
wako tayari kuendelea kushirikiana na serikali.
Kuhusu
mbegu alisema kuwa itafanya uchunguzi na kuangalia mifumo yake na namna
ya kushirikiana na wadau katika udhibiti wa mbegu bora hapa nchini.
Alisema
uwepo wa mbegu feki unaathiri kwa kiasi kikubwa wafanyabiashara na
wakulima wanapopata mbegu hizo zinawaathiri na kushindwa kupata mazao
waliyoyategemea na kuwa mbegu bora zinatoa uhakika wa chakula na usalama
wa nchi.
Kupatikana
kwa mbegu bora kunaandaa mazingira mazuri ya biashara hivyo usambazaji
wa mbegu na uwepo wa mbegu feki katika masoko unaathiri wafanyabiashara,
mbegu feki zinapomfikia mkulima zinatuathiri sana hawapati mazao
tunayoyategemea”, alisema
“Jambo
hili tunaenda kulifanyia kazi kwa kufanya uchunguzi na kuangalia mifumo
yetu ya serikali ni jinsi gani inaweza kuahirikiana kudhibiti mbegu
hizo na kama mna majawabu kwenye masuala hayo serikali ipo tayari
kusikia na kuyafanyia kazi,”
Balozi
wa Uholanzi nchini Tanzania Wiebe De Boer,alisema madhumuni ya mkutano
huo ni kujadili hali ya mbegu bora nchini Tanzania na matumizi ya mbegu
bora,kuangalia changamoto zinazokabili sekta hiyo na namna ya kuzitatua
ili kuiboreshaji wa sekta hiyo ambayo ni muhimu katika kuongeza mavuno
na usalama wa chakula.
Alisema
faida za upatikanaji na matumizi ya mbegu bora,uboreshwaji wa mazingira
ya biashara katika sekta hiyo utasaidia kukuza sekta hiyo na kuwa nchi
hiyo iko tayari kutoa utaalamu wake juu ya masuala ya mbegu wakiamini
kuwa mavuno mazuri huanza na mbegu bora.
Alisema
anafurahi kuona wataalamu wengi wa masuala ya mbegu wakikutana kwa
pamoja na kujadiliana juu ya namna ya kuboresha sekta hiyo.
Alisema serikali ya nchi yake itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania na sekta binafsi katika kukuza kilimo.
Naye
Mkurugenzi wa Kanda wa Kituo hicho, Dk Gabriel Rugalema,alisema
upatikanaji na matumizi bora ya mbegu ni muhimu kwa ukuaji wa nchi
yoyote.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara wa Mbegu
Tanzania(Tasta),Bob Shuma,alisema kazi yao kubwa ni kushirikiana na
serikali kwa kuhakikisha nia za serikali na wawekezaji zinakamilika na
wananchi wanapata mbegu bora.
Alisema
kunapokuwa na chakula kingi katika nchi ni kwa sababu ya ushirikiano
baina ya serikali na sekta binafsi ambazo kwa pamoja zinahakikisha
mkulima anapata mahitaji yake.
“Pamoja
na mambo mengine tumejadili na kuhakikisha ubora wa mbegu ambazo
zinazalishwa hapa nchini zinapelekwa nje ya nchi pamoja na zile
zinazouzwa hapa nchini,”alisema
“Ubora
wa mbegu ni muhimu hivyo lazima tuweke mifumo mizuri,tumeangalia
tumetoka wapi,tumefika wapi na tunaelekea wapi kuhakikisha yaliyofanyiwa
kazi yatazidi kuwepo na utafiti unaongezeka,tumezungumzia juu ya
wawekezaji wa ndani kwa mfano tuna makampuni za wazawa walioanzisha
kampuni za mbegu
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )