Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, June 13, 2022

Tanzania na Oman kukuza uhusiano wa kibiashara


Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania itaendelea kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara uliojengeka kwa muda mrefu baina yake na Oman.
 
Rais Samia ameyasema hayo nchini Oman wakati wa kongamano la wafanyabiashara wa Tanzania na Oman, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu nchini humo.
 
Akiwa nchini Oman Rais Samia Suluhu Hassan pia ameshuhudia utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano katika sekta mbalimbali.

Amewakaribisha wawekezaji wa Oman kuwekeza Tanzania kwenye sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na utalii, kilimo, uvuvi, madini na ufugaji.  
 
Kwa mujibu wa Rais Samia Suluhu Hassan, serikali inaendelea kurekebisha sheria na makosa yaliyojitokeza katika sekta ya uwekezeji na kuweka mazingira rafiki kwa ajili ya uwekezaji nchini.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: