Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, June 26, 2022

Urusi kupeleka mfumo unaofyatua makombora ya nyuklia Belarus


Rais wa Urusi Vladimir Putin ameahidi kupeleka mifumo ya Iskander-M inayoweza kufyatua makombora ya nyuklia nchini Belarus. Haya yamejiri mnamo wakati vikosi vya Urusi vimechukua udhibiti kamili wa mji wa Sieverodonetsk.

Urusi inanuia kupeleka mifumo kwa jina Iskander-M inayoweza kufyatua makombora ya nyuklia nchini Belarus katika miezi michache ijayo. Rais Vladimir Putin alisema hayo Jumamosi kupitia televisheni ya Urusi wakati wa kuanza kwa mkutano kati yake na kiongozi wa Belarus Alexander Lukashenko mjini Saint Petersburg.

Putin alisema pia Urusi itaisaidia Belarus kuboresha ndege zake za kivita aina ya Su-25 kuziwezesha kubeba silaha za nyuklia.

Rais wa Belarus Lukashenko alielezea wasiwasi wake kuhusu kile alichokiita uchokozi na serĂ¡ za kuudhi za majirani zake Lithuania na Poland.

Alimuomba Putin kuisaidia Belarus kuwa na ‘majibu yanayofanana' na kile alichosema kuwa ndege za kivita za nyuklia zinazoongozwa na Jumuiya ya Kujihami ya NATO, karibu na mpaka wa Belarus

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: