Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, June 25, 2022

Watuhumiwa watatu wa ujambazi wauawa


 Watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wameuawa katika eneo la Goba wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam, wakati wa majibizano ya risasi na polisi.

Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Muliro Jumanne amewaambia waandishi wa habari kuwa, watu hao walikuwa katika harakati za kuiba kwenye duka linalojulikana kama Sky Matty.

Amesema polisi walifanikiwa kuwadhibiti watuhumiwa hao wa ujambazi kutokana na ushirikiano walioupata kutoka kwa wananchi.

Kwa mujibu wa kamanda Muliro, askari mmoja amejeruhiwa katika tukio hilo na kwa sasa anaendelea kupatiwa matibabu.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: