WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe, amewahakikishia wadau wa Sekta ya Kilimo kuwa kipaumbele cha Serikali ni kuimarisha Sekta ya Kilimo cha umwagiliaji ili kupunguza adha ya kutegemea kilimo cha mvua.
Ameyazungumza
hayo Mkoani Morogoro wakati anafungua mkutano wa wadau wa kilimo cha
Umwagiliaji ulioandaliwa na Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Tume ya
Taifa ya Umwagiliaji Juni 15, 2022.
Waziri
Bashe amesema katika bajeti ya fedha ya mwaka 2022/23, Serikali
imetenga shilingi Bilioni 364 katika Sekta ya Kilimo cha Umwagiliaji,
pia kuna ongezeko la Bilioni 50 ambazo zimetengwa ili kuleta mafanikio
chanya katika Sekta hiyo.
Aidha Serikali kupitia Wizara ya Kilimo itatangaza hekta elfu 10 kwa ajili ya Kilimo cha Umwagiliaji.
Waziri
Bashe ameongeza kuwa kutokana na Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa na utashi wa kisiasa katika
Sekta ya Kilimo, Serikali imedhamiria kuwekeza katika kilimo cha
Umwagiliaji.
Serikali
imetenga hekta Elfu 20 kwa ajili ya mashamba ya Vijana ambayo
yatatengenezewa miundombinu ya Umwagiliaji ili kupunguza tatizo la ajira
nchini.
Waziri
Bashe alimalizia kwa kuwa Serikali imefungua milango kwa wadau wote wa
Sekta ya Kilimo kupeleka mawazo yatakayochochea matokeo chanya na kuinua
Sekta ya Kilimo nchini.
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )