JESHI la polisi
Mkoani Pwani , linamshikilia mtuhumiwa wa mauaji ya mtoto wa miaka Saba
,ambae amebakwa na kuuwawa Mei 30 mwaka huu ,Misugusugu wilayani Kibaha .
Kaimu Kamanda wa
polisi Mkoani hapo ,Gregory Mushi alisema mtuhumiwa huyo anadaiwa
kufanya tukio Hilo la kinyama kisha kukimbia .
Anasema ,mkono wa
sheria Ni mrefu , Jeshi Hilo limefanikiwa kumkamata ili aweze
kuchukuliwa hatua za kisheria ,iwe fundisho kwa wengine.
Aidha ,Mushi alitaja
tukio jingine lililohusisha mtoto wa kike miaka 5 mwanafunzi wa
chekechea kumwagiwa mafuta ya kula ya Moto na mfanyakazi wa ndani aitwae
Rehema anaekadiriwa Kuwa na miaka 14 mkazi wa Mbwewe Chalinze.
“Mtoto huyu amejeruhiwa usoni na mkono wa kulia ,,Tumemkamata baba mzazi wa mtoto baada ya kumtorosha mtuhumiwa”
Katika tukio jingine
,Mushi alieleza , jeshi la polisi kwa kushirikiana na Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) mkoa limemkamata mtu mmoja mwanaume (39) mkazi wa
Mlandizi akiharibu miundombinu ya Tanesco na kuipatia hasara ya zaidi
ya milioni 76 huko Vikuruti kata ya Mlandizi.
Alisema ,mtu huyo amekata line ya umeme ya msongo wa 33KV ambao ulikuwa unamhudumia mteja aliyetambulika kwa jina la Swai.
“Kilichotumika Ni
kwamba ilichomwa Moto nguzo na kusababisha line hiyo kuanguka na kuiba
waya wa alminium ACCR 100 MM2 na kulisababishia hasara ya sh.milioni
76.896.108 .
Tukio la tatu
,kusafirisha mirungi ambapo polisi walifanya msako kumkamata mtu mmoja
eneo la Chalinze akisafirisha mirungi bunda 150 zenye uzito wa kg 70
kutoka Moshi mkoa wa Kilimanjaro kuelekea Tunduma wilaya ya Momba mkoa
wa Songwe kwa kutumia gari lenye namba za usajili T.254DDY Sina ya
Toyota Ipsum.
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )