Rais wa Marekani Joe Biden ameahidi leo kuwa nchi yake itatumia "nguvu zote ilizo nazo" kuizuia Iran kumiliki silaha za nyuklia.
Biden ametoa ahadi
hiyo baada ya kujiunga na waziri mkuu wa Israel Yair Lapid mjini
Jerusalem kutia saini mkataba wa ushirikiano unaosisitiza nia ya
Marekani ya kuendelea kuisaidia Israel kujilinda dhidi ya kile kinatajwa
kuwa kitisho kwa dola hiyo ya kiyahudi.Waziri mkuu wa Israel ameusifu
mkataba huo mpya na dhamira iliyoelezwa na Biden.
Chini ya mkataba huo
uliosainiwa wakati wa siku ya pili ya ziara ya Biden nchini Israel,
Marekani pia inatoa hakikisho la kuyakabili makundi ya wanamgambo yenye
mafungamano na Tehran.
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )