Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, July 6, 2022

Haji Manara amuomba radhi Rais Karia


Afisa habari wa Yanga Haji Manara amemuomba msamaha Rais wa TFF Wallace Karia kutokana na tukio lililotokea Jijini Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati wa mechi ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam.

Mara baada ya mchezo huo kuna video iliyosambaa mitandaoni ikimuonesha Afisa huyo wa Yanga akijibizana au kutupiana maneno na Rais wa TFF Wallace Karia huku wengi wakitafsiri kuwa Manara alikuwa akimtukana Rais huyo.

Akiongea na waandishi wa habari  Manara amesema kuwa alikosea kujibizana na Rais hadharani huku akiweka wazi kuwa yupo tayari kuwajibishwa iwapo itaonekana. Inastahili.

''Nilienda kumuona rais wa TFF nyumbani kwake,  kumuomba radhi juu ya kilichotokea naamini mimi nikama mwanae natumaini atakuwa amenielewa"amesema Haji Manara.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: