Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, July 10, 2022

NEC yamteua Tamima Haji kuwa Mbunge Viti Maalum CCM


 TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC) imemteua, Tamima Haji Abass kuwa Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imefanya uteuzi huo kufuatia kikao chake cha  Julai 9, 2022 kwa kuzingatia matakwa ya ibara ya 78 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 ikisomwa pamoja na kifungu cha 86A (6) na (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.
 
Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa  Julai 9, 2022 na Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Dkt.Wilson Mahera Charles.

Amesema, uteuzi huo umefanyika baada ya tume hiyo kupkea barua Mei 12, 2022 yenye Kumb. Na. CEB. 137/400/02A/10 kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoandikwa kwa mujibu wa kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.

Barua hiyo ilitaarifu kuhusu uwepo wa nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mheshimiwa Irene Alex Ndyamkama.Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: