Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, July 7, 2022

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ajiuzulu


Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amekubali kujiuzulu, na kumaliza mgogoro wa kisiasa usio wa kawaida juu ya mustakabali wake. 

Haikubainika wazi mara moja ikiwa Johnson atabaki ofisini wakati chama cha Conservative kikichagua kiongozi mpya ambaye atachukua nafasi yake kama waziri mkuu. 

Afisa mmoja kutoka ofisi ya Johnson ya Downing Street amethibitisha kuwa waziri huyo mkuu atatangaza kujiuzulua kwake baadaye. 

Afisa huyo alizungumza kwa sharti la kutotambulishwa kwasababu bado hatua hiyo ya kujiuzulu haijatangazwa rasmi. 

Wakati huohuo, chama kikuu cha upinzani cha Labour nchini Uingereza, kimesema kuwa matarajio ya kujizulu kwa Johnson kama waziri mkuu ni habari njema. 

Lakini mbunge wa chama hicho Keir Starmer ameongeza kuwa kubadilisha kiongozi wa chama cha kihafidhina hakutoshi na kwamba wanahitaji mabadiliko yanayofaa ya serikali.

Tangazo
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

End: