Saturday, October 8, 2011

AUNT LULU APARAMIA POMBE NA KUFANYA MAMBO YASIYO NA HESHIMA HADHARANI


Mtangazaji mahiri wa  Bongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’ amenaswa akiwa hoi kwa kilevi na kuwaacha wadau midomo wazi


Kituko ni kwamba, Aunty Lulu alifakamia pombe hizo zilizompeleka hali ya ‘u-tilalila’ katika kipindi hiki ambacho anakabiliwa na mitihani ya kumaliza masomo ya uandishi wa habari ngazi ya stashahada.


Staa huyo aliyeanza ‘kuhiti’ tangu akiwa na umri mdogo, alinaswa na MPEKUZI  wetu  usiku wa Jumatano iliyopita ndani ya Club Bilicanas, Dar es Salaam.


Ilikuwa saa 6:39, ambapo mpekuzi wetu  alimtia machoni Aunty Lulu kwa mara ya kwanza ndani ya klabu hiyo, kulikokuwa na shoo ya Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’.
 

Wakati huo, staa huyo alikuwa akirandaranda mfano wa mtu aliyekuwa akitafuta sehemu ya kujiegesha.
Baada ya kuzunguka kwa dakika mbili hivi, Aunty Lulu alitenga makalio jirani na moja ya kaunta za klabu hiyo na kuanza kupiga pombe  ambayo ilimchakaza na kumuacha hoi.Kabla hajazimika, Aunty Lulu alifanya vitu viwili kwa zamu akiwa tayari rojorojo, kunywa pombe kwa fujo na kuchangamka kwa muziki wa Twanga, hivyo kukata mauno ‘kama hana akili nzuri’.


Kama ilivyo kwa msemo, ‘ulevi noma, funda moja tu la ziada linaweza kukuumbua’ ndivyo mambo yalivyomtokea puani Aunty Lulu, kwani mwisho alikuwa taabani na kufanya yasiyo na heshima.
Moja ya matukio ya kilevi aliyoyafanya ni kumvamia jamaa mmoja (pichani juu) na kudendeka naye bila woga kabla ya kulala fofofo kwa kuugeuza ubao wa kaunta ndiyo kitanda cha chumbani kwake

 
Baadhi ya watu wanaomfahamu Aunty Lulu waliamua kumuokoa kwa kumpakia kwenye teksi ili kumrudisha nyumbani kwao.Baada ya kupigiwa simu siku ya alhamisi ili kumjulia hali  kutokana na jana yake kuwa tilalila alijibu:
“Jamani mimi sikumbuki kitu, rafiki zangu ndiyo wameniambia asubuhi hii. Nadhani pombe sasa zinanishinda, hii ni hatari.”


BREAKING NEEEEWZ


MBINU 5 ZA KUMTAMBUA MWANAMKE ANAYEKARIBIA KUMUACHA MWANAUME.  << BOFYA HAPA>>

 


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )