Tuesday, September 17, 2013

Hii ndo bunduki iliyotumika katika mauaji ya Bilionea Erasto Msuya....Watuhumiwa wakimbilia kwa Sangoma

 
 Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akionesha bunduki iliyokamatwa mbele ya waandishi wa habari(hawako pichani)inayodaiwa kutumika katika mauaji ya bilionea wa madini Erasto Msuya.
 Bunduki inayodaiwa kutumika katika mauaji hayo.
Pikipiki mbili zinazodaiwa kutumika katika mauaji ya bilionea wa madini Erasto Msuya.
*******************
JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro limefanikiwa kunasa bunduki aina ya SMG yenye namba za usajili  KJ10520  inayoaminika kutumika katika mauaji ya mfanyabiashara bilonea wa madini ya Tanzanaiti , Erasto Msuya (43) aliyeuawa kwa kupigwa risasi 13 kifuani Augosti 7 mwaka huu Mijohoroni wilayani Hai.


Mbali na bunduki hiyo jeshi hilo pia limefanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa wengine wanne wanaodaiwa kuwa ni watuhumiwa muhimu katika mipango ya mauaji ya mfanyabiashara huyo anaye aminika kuwa na vitega uchumi vya kutosha katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.


Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake,kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro,Robert Boaz,aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni ,Sadick Mohamed Jabir(32) mkazi wa jijini Dar es salaam na Lang’ata

wilaya ya Hai na Karim Issa Kihundwa(33) mkazi wa Lawate wilayani Siha ambao wanatajwa kuwa ni muhimu katika mauaji hayo.


Alisema watuhumiwa hao wawili walikamatwa  eneo  la Kaliua wilaya ya Sikonge mkoani Tabora wakiwa kwa mganga wa kieneyeji wakifanyiwa zindiko ili wasitiwe mbaroni  na baada ya kuhojiwa na polisi walieleza jinsi walivyoshiriki mauaji hayo na mahali walipoficha silaha na pikipiki zilizotumika katika tukio hilo.


Boaz aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Jalila Zuberi  Said(28) mkazi wa Babati mkoani Manyara pia anaishi wilaya ya kondoa mkoani Dodoma na Joseph Damas Mwakipesile maarufu kwa jina la ‘Chusa’(35) ambaye pia ni mfanayabiashara wa madini ya Tanzanite anayeishi Jijini Arusha ambaye anashikiliwa na jeshi hilo kwa zaidi ya wiki mbili sasa.


Alisema jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata pikipiki nyingine inayodaiwa kutumika katika tukio hilo yenye namba za usajili T751 CKB aina ya KINGLION rangi nyeusi  ambayo wakati wa tukio ilikuwa ikitumia namba za bandia.


Kamanda Boaz alisema Bunduki iliyokamatwa ilikutwa ikiwa imefichwa kwneye tindiga katika eneo la Boroi kwenye mpaka  wa wilaya za Hai na Siha huku akiendelea kutoa  wito kwa wananchi wapenda  amani mkoani Kilimanjaro,kuendelea kutoa ushirkiano kwa jeshi hilo katika kukomesha uharifu.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )