Sunday, March 27, 2016

Rais Magufuli aitakia heri Taifa Stars dhidi ya Chad


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameitakia heri timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) katika mchezo wake dhidi ya Timu ya Taifa ya Chad, utakaofanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam, kesho tarehe 28 Machi, 2016. 

Taifa Stars itacheza mchezo huo wa marudiano, ikiwa ni wiki moja tangu ilipocheza mchezo wa kwanza, katika Jiji la N’Djamena nchini Chad ambapo Taifa Stars ilishinda bao 1–0. 

Katika salamu hizo Rais Magufuli amewataka wachezaji, benchi la ufundi na viongozi  wa Shirikisho la Soka hapa nchini (TFF), kutambua kuwa watanzania wana matumaini makubwa kuwa timu yao itafanya vizuri katika mchezo huo, ikiwa ni  juhudi za kutafuta tiketi ya kufuzu kucheza fainali za kombe la soka barani Afrika, zitakazofanyika Gabon hapo Mwaka ujao wa 2017.
 
“Watanzania wote tuiombee timu yetu ifanye vizuri ushindi wa Taifa Stars ni heshima kwa nchi yetu na sifa muhimu kimataifa mimi naamini kama tulishinda N’Djamena tunao uwezo wa kushinda hapo kesho” amesisitiza Rais Magufuli 

Gerson Msigwa 
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam 
27 Machi, 2016
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )