Friday, March 18, 2016

Umoja wa Rufaa za Wananchi Tanzania Wawaomba Wazanzibar Wajitokeze Kwa Wingi Kupiga Kura Tarehe 20

Viongozi wa muungano wa vyama vya siasa uitwao Umoja wa Rufaa za Wananchi Tanzania wamewaomba Wazanzibari kukamilisha haki yao ya kupiga kura katika uchaguzi wa marudio ili wapate viongozi wa kuwaletea maendeleo

Ujumbe wa watu saba wa umoja huo ukiongozwa na John Shibuda wa Ada Tadea, ulitoa kauli hiyo jana ulipokutana kwa mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, ilisema ujumbe huo ni kutoka vyama visivyokuwa na wabunge ambavyo ni UPDP, Sau, UDP na Ada-Tadea.

Msimamo wa vyama hivyo unakinzana na ule wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) uliotoa tamko la kususia uchaguzi huo wa marudio.

Kwa upande wake John Cheyo alisema upigaji kura ndiyo njia pekee itakayotoa mwanga kwa wananchi wa Zanzibar kuamua wapi wanataka kuelekea katika mustakabali wa maisha yao ya baadaye.

Wakati huohuo, vyama 12 visivyo na uwakilishi bungeni vimetoa tamko la kushiriki uchaguzi huo vikisema hoja za kugomea uchaguzi huo hazina mashiko.

 Vyama vilivyotoa tamko hilo ni CCK, Sau, Ada-Tadea, TLP, AFP, UPDP, Demokrasia Makini, NRA, UMD, Chausta, DP na ADC ambacho mgombea urais Zanzibar ni Hamad Rashid aliyejiengua CUF miaka miwili iliyopita. 

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )