Wednesday, April 20, 2016

Bungeni: Kujitoa MCC Hakutaathiri Mradi wa Usambazaji Umeme


Serikali ya Tanzania imesema kujitoa kwa wafadhili wa Shirika la Changamoto za Milenia(MCC),katika miradi ya kuzalisha umeme hukujaathri utekeezaji wa miradio hiyo ya usambazaji wa umeme vijijini.

Akitoa kauli hiyo ya Serikali jana Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha Maswali na Majibu Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani, amesema miradi yote ya shirika hilo ya awamu ya kwanza ilitekelezwa vizuri na kukamilika.

Dkt. Kelemani amesema kuwa katika utekelezaji wa miradi hiyo awamu ya pili serikali itatoa shilingi bilioni moja na kiasi kingine kitatolewa na benki ya Maendeleo ya Afrika AFDB na Benki ya dunia (WB).

Dkt. Kilimani amesema tayari Bank ya Maendeleo ya Afrika imesema itatoa shilingi bilioni moja Dola za Marekani na vilevile Benki ya dunia itatoa shilingi bilioni 3 dola Marekani ili kukamilisha mradio huo kwa awamu ya tatu kwa hiyo mradi huo hautatetereka.

==> Zaidi, bonyeza hapo chini kumsikiliza
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )