Thursday, April 14, 2016

Mwakyembe: Bora Tufe Masikini Kuliko Kuwapigia Magoti Wazungu


DK. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Katiba na Sheria, amesema kuwa Tanzania ni bora iendelee kutaabika na watanzania wafe wakiwa masikini kuliko kuendelea kunyanyaswa na mataifa ya ulaya.

Mwakyembe ambaye hata hivyo hakuyataja mataifa hayo lakini moja kwa moja ilionekana kuyagusa baadhi ya mataifa ya Ulaya pamoja na Serikali ya Marekani iliyovunja uhusiano na Serikali ya Tanzania katika mambo yote yanayohusu miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na mfuko wa changamoto za millenia (MCC).

Mwakyembe ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na watumishi wa wizara ya katiba na sheria jijini hapa, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi kwa mkoa wa Mwanza.

Mwakyembe ambae pia ni mbunge wa Jimbo la Kyela mkoani Mbeya, amesema kuwa anashangazwa na baadhi ya watu wanaotaka kuliingiza taifa katika mambo mabaya yasiofaa na yalioko kinyume na maadili ya watanzania.

Amesema mataifa hayo yamekuwa yakionekana kuilazimisha Tanzania kuingia katika mambo yasiyokubalika na watanzania wenyewe ikiwemo suala la `ushoga` kitendo ambacho alidai ni cha hovyo.

“Ni bora tufe masikini kuliko kuendeshwa kwa hofu, wao wanataka watuendeshe tu, sisi vitu kama vya ushoga vinapaswa kupingwa vibaya na haiwezekani kabisa.

“Vitu kama vya ushoga ni vya hovyo na kama watanzania hatukubaliani navyo, hata maadili yetu yenyewe hayataki mambo kama hayo,” amesema Mwakyembe.

Machi 29 mwaka huu, Serikali ya marekani kupitia kwa bodi ya wakurugenzi wa MCC ilitangaza uamuzi wa kuinyima Serikali Dora za kimarekani Milioni 472.8 ( zaidi ya Sh. Trioni 1 na bilioni 20) kutokana na marudio ya uchaguzi wa serikali ya Zanzibar na sheria ya makosa ya mtandao. 

Hata hivyo, Marekani kupitia kwa balozi wao hapa nchini Mark Childress, jana ilionyesha kulegeza msimamo wao ambapo walisema wataendelea kuisaidia Tanzania hasa katika sekta ya Afya  na  Elimu licha ya changamoto za kisiasa zilizopo

Mahakimu  mizigo  kukiona
Katika hatua nyingine Waziri Mwakyembe, amesema kuwa ofisi yake tayari imekwishaunda kamati za madili za Mahakama, ili kudhibiti baadhi ya mahakimu wanaofanya kazi kwa mazoea na kutokufata maadili.

Amesema kuwa kuundwa kwa kamati hiyo, kutasaidia watu kufanya kazi kwa kuzingatia weledi wa fani hiyo muhimu nchini kwani kuna baadhi ya mahakimu walevi wasiofuata maadili ya kisheria.

“Tuna taarifa wapo baadhi ya mahakimu ambao ni walevi na wengine wanafikia hatua ya kupewa msaada baada ya kuzidiwa na pombe lakini sasa kesho unashangaa huyo hakimu anakuja na yeye kutoa uamzi,” amesema Mwakyembe.

Amesema kuwa lengo jingene la kuunda kamati hiyo ni kutaka kurekebisha baadhi ya tabia za mahakimu wakiwemo wa Mahakama za mwanzo kutenda haki kwa Wananchi wote bila kumpendelea mtu.

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )